Entertainment

Vitabu vya historia vya ligi kuu ya England hususan timu za Chelsea na Liverpool vinatarajia kufungwa mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo wachezaji wawili wa zamani wa timu ya taifa ya England watakapokuwa wanazichezea klabu zao kwa mara moja ya mwisho .
Frank Lampard ambaye anacheza kwa mkopo kwenye klabu ya Manchester City toka klabu ya New York City Fc iliyomsajili toka Chelsea na mwenzie Steven Gerard wa Liverpool wanatarajiwa kupunga mkono wa kwaheri kwa ligi kuu ambapo watakuwa wanachezea klabu zao kwa mara ya mwisho.
Gerard na Lampard wameziwakilisha klabu zao kwenye michezo zaidi ya 500 kwenye ligi ya England kwa kila mmoja huku wakifunga zaidi ya mabao 100.
Gerard na Lampard wameziwakilisha klabu zao kwenye michezo zaidi ya 500 kwenye ligi ya England kwa kila mmoja huku wakifunga zaidi ya mabao 100.
Viungo hawa wawili watabadilisha viwanja toka nchini England kwenda Marekani ambako Steven Gerard atakuwa anaichezea Los Angeles Galaxy huku Lampard akichezea New York City Fc .
Gerard anaondoka Liverpool akiwa na rekodi ya kutwaa mataji yote kasoro taji la ubingwa wa ligi ya England huku Frank Lampard akiwa amepata mafanikio zaidi kwa kutwaa mataji karibu yote pamoja na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora katika historia ya Chelsea.
Lampard na Gerard wanaihama ligi ya England na watahamia nchini Maekani .
Lampard na Gerard wanaihama ligi ya England na watahamia nchini Marekani 
Katika miaka zaidi ya 10 ya kucheza ndani ya Chelsea Frank Lampard amecheza jumla ya mechi 608 huku akifunga mabao 176 na Gerard kwa upande wake amecheza mechi 503 na amefunga mabao 119 rekodi hizi zikiwa kwenye ligi kuu ya England pekee .




About qwerty

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Top