Wenyeji Chile wametinga hatua ya fainali ya Copa America baada ya kuifunga timu pungufu ya Peru magoli 2-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Santiago.
Eduardo Vargas ameifungia Chile magoli mawili katika dakika ya 42′ na 64′, lakini dakika ya 60′ Mlinzi Gary Medel alijifunga bao na kuwapa angalau ahueni Peru.
Mapema dakika 20′ Mwamuzi wa mechi, Jorge Argote alimuonesha kadi nyekundu (Umeme) Carlos Zambrano kwa kosa la kumkanyaga mgongoni kiungo wa Chile,Charles Aranguiz.
Chile watacheza fainali na Argentina au Paraguay ambao wanakutana leo majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika mechi ya pili ya nusu fainali.
Source: shaffihdauda.com
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com