Imekuwa utamaduni wa klabu mbalimbali barani ulaya kuzindua jezi mpya kila msimu ambapo jezi hizi huingia sokoni na kuuzwa kwa mashabiki wa klabu husika huku klabu hiyo ikijiingizia kipato ambacho husaidia kwenye uendeshaji wa shughuli zake .
Manchester United inatarajiwa kuzindua jezi mpya siku za hivi karibuni ambapo zitakuwa jezi ambazo zimetengenezwa na mdhamini mpya wa klabu hii ambaye ni Adidas . Adidas wameingia mkataba na United baada ya klabu hiyo kumaliza mkataba wake wa muda mrefu na kampuni ya Nike.
Jezi mpya za United zitakazotumika msimu ujao zimevuja kwenye mtandao wa Internet ambapo picha ya mchezaji Ashley Young imeonekana ambapo mchezaji huyo ni kama amepozi akiwa anapigwa picha maalum kwa ajili ya matangazo ya jezi hizo .
Hata hivyo United haijatoa taarifa rasmi kuhusu uzinduzi wa jezi mpya na kilichoonekana ni picha ambayo wengi wameihusisha na jezi ambazo United itazindua siku za karibuni.
Toa maoni yako hapa chini kuhusu Jezi hizi.