Thamani ya United imeongezeka maradufu kutokana na mikataba kadhaa ya
udhamini na biashara ambayo imekuwa ikiingia kila mara chini ya uongozi
wa Mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward.
Chini ya uongozi wake thamani ya United imekuwa kubwa hali ambayo
imefanya timu hii kuwa na fedha ambazo zinaipa kiburi cha kuwa na uwezo
wa kufanya usajili wa nguvu bila kuhofia minyororo ya kanuni ya
financial fair play.
Real Madrid wanashika nafasi ya tatu katika orodha hiyo
United inafuatiwa na klabu za Bayern Munich na Real Madrid ambazo zimefuatana katika orodha kwenye nafasi ya pili na ya tatu huku Manchester City na Chelsea zikikamilisha orodha ya 5 bora .
Fc Barcelona ambayo ubingwa wa ulaya iliyoutwaa juzi umeiongezea
kipato cha paundi milioni 28 iko kwenye nafasi ya sita nyuma ya Man City
.
Sababu kubwa ya kupanda kwa thamani ya Manchester United ni
Mkurugenzi wake Ed Woodward ambaye chini ya uongozi wake klabu hii
imeingia mikataba mingi yenye thamani kubwa .
ORODHA KAMILI YA CLUB ZENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI
ORODHA KAMILI YA CLUB ZENYE THAMANI ZAIDI DUNIANI