Anauzoefu mkubwa wa ligi ya Uingereza baada ya kucheza mechi zaidi ya 300 na kushinda mataji. Viera ambae wiki hii amekamilisha mafunzo yake ya leseni ya kuwa professional kocha iliyoandaliwa na UEFA anaweza kuwa kocha msimu ujao kwenye EPL.
Kwa sasa hivi Patrick Viera anafanya kazi na Manchester city kama kocha wa kikosi cha chini ya miaka 21 anapigiwa chapuo kukiongoza kikosi cha Newcastle kwenye msimu wa 2015/2016.
Taarifa kutoka Sky Sport zinasema kwamba Viera anatarajiwa kuchaa na uongozi wa Newcastle mapema wiki ijayo kwa ajili ya kuzungumza kuhusu yeye kuwa kocha mpya.
Newcastle wanatafuta kocha mdogo mwenye njaa ya mafanikio ambae pia atafanya kazi ya kukijenga kikosi chao. Patrick Viera amepewa nafasi pia kwenye hii kazi.