Klabu ya Real Madrid imemthibitisha Mhispania Rafael Benitez kama kocha wake mpya zikiwa zimepita siku mbili tangu kocha huyo alipoachana na klabu yake ya zamani ya Napoli.
Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid , ana historia ndefu ndani ya klabu hiyo akiwa amewahi kuichezea akiwa kwenye kikosi cha vijana kabla ya kuwa kocha wa timu za vijana na baadae kikosi cha kwanza akiwa chini ya Vicente Del Bosque.
Madrid imethibitisha kuwa Bneitez ametia saini mkataba wa miaka mitatu na ataanza kazi yake mara tu baada ya mapumziko baada ya msimu wa ligi za soka barani ulaya kumalizika.
Hivi karibuni Real Madrid ilitangaza kuachana na kocha wake Carlo Ancelotti baada ya kumaliza msimu bila taji lolote.
Kwa muda mrefu tetesi zilimhusisha Benitez na kujiunga na Real ambapo siku hadi siku tetesi hizo zilizidi kupata nguvu mpaka hii leo ambapo imethibitika rasmi kuwa Benitez ndio kocha mpya wa Real Madrid .
Kabla ya Real Madrid , Benitez aliwahi kuwa kocha wa Valencia , Liverpool , Inter Milan , Chelsea na Napoli ambako akiwa na Valencia , Chelsea , Liverpool na Inter Milan amewahi kutwaa mataji makubwa ikiwemo ligi ya Hispania , Lii ya mabingwa , ligi ya UEFA Europa na kombe la dunia kwa klabu.
Toa maoni yako hapa chini kuhusiana na habari hii.