Ijumaa iliyopita, Sky Sports walidai kwamba Cech angesaini Emirates siku hiyo, lakini haikutokea.
Mashabiki wa Arsenal wamechoka kusikia tetesi inayotangaza kwamba watamsajili golikipa wa Chelsea, Petr Cech, lakini siku ya kufanya hivyo haijulikani.
Kwa wiki kadhaa, taarifa zimekuwa zikitoka kuwa Cech anaweza kusaini leo, lakini hiyo leo haifiki.
Hii inazua wasiwasi kama kweli Cech atajiunga na Arsenal majira haya ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 11.
Hata hivyo, Jose Mourinho hapendi kuona kipa huyo anajiunga na wapinzani wake wa ligi kuu England, lakini mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amemruhusu Cech kuondoka na amemshukuru kwa kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio.
Leo kuna Tweet moja kutoka kwa mwandishi wa gazeti la Dail Telegraph, Jason Burt akithibitisha kwamba Cech atajiunga na Arsenal kesho Jumatatu, lakini baadhi ya watu wamemjibu …
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com