Ikiwa ni saa chache baada ya Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatterkutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa huo kuna habari nyingine zinamuhusu Rais huyo.
Rais huyo ambaye alipewa madaraka ya kuongoza Shirikisho hilo siku chache zilizopita ikiwa ni awamu ya tano, kingine kilichochukua Headlines kwa sasa ni ishu ya Sepp Blatter kufanyiwa uchunguzi na maafisa wa Marekani ili kujua kama anahusika na tuhuma za rushwa ambazo zinawahusu maafisa wengine saba wa FIFA.
Hata hivyo Blatter amesema ataendeleaa kukaa madarakani hadi utakapoitishwa mkutano wa kumpata Rais mwingine kati ya December 2015 na March 2016.