SHINJI KAGAWA AIAGA RASMI MANCHESTER UNITED NA KURUDI ALIPOTOKA
Yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya dirisha la usajili kufungwa, taarifa mpya ni kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ameihama klabu hiyo.
Kagawa aliyejiunga na Man United misimu miwili iliyopita amerudi kwenye klabu aliyotoka ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani.
Man United walimnunua Shinji kwa ada ya uhamisho wa £12m na leo hii imethibitishwa kwamba amejiunga na Dortmund kwa £8m.
Wakati huo huo mwanasoka wa Uholanzi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Ajax Daley Blind amefanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Man United kwa ada ya £13m.