Ni miaka sita imepita tangu Rais Obama amekabidhiwa Ikulu ya White House na kuwa Rais wa nchi hiyo.. labda umewahi kuona Tweets kwenye account ya Obama, lakini kumbe tweets hizo hata hakuhusika kuandika!!
Sasa Obama amekabidhiwa rasmi kuendesha ukurasa wake mpya wa Twitter yeye mwenyewe.
Idadi ya followers alionao ni Mil. 1.99 mpaka sasa hivi ambapo ni siku mbili tangu ifunguliwe na kila wakati idadi ya followers inaongezeka kwa sababu watu wengi wanaendelea kumfollow baada ya kufikiwa na hii stori kwamba ukurasa huo uko mikononi mwake kwa sasa.
Tweet ya kwanza aliandika hivi>>”Hello, Twitter! It’s Barack. Really! Six years in, they’re finally giving me my own account“>> @POTUS (President of the United States)
Tweet nyingine ni hii ya chart yake na Bill Clinton>> “Good question, @billclinton. The handle comes with the house. Know anyone interested in @FLOTUS?>> @POTUS
Taarifa ya Ikulu ya White House wamesema wameamua kumuachia Obama aiendeshe account yake mwenyewe ili ajiandae na maisha ya uraiani ambapo amebakiza muda mfupi kabla ya kustaafu, kingine ni kumsogeza jirani zaidi na na watu wake wa Marekani.
Idadi ya Tweets alizoandika mpaka sasa ni tatu tu, na watu anaowa'follow yeye ni 65.