Mlango mwingine ni huu unafunguka kwenye historia ya Entertainment Tanzania !! Tayari duniani wanatujua kwa Tuzo nyingi ambazo zimebebwa na mastaa kama AY, Vanessa Mdee na Diamond Platnumz.. Kama bado hujajua ni kwamba mwaka huu pia kuna jina la Mbongo wetu mmoja kwenye walioteuliwa kwenye Tuzo za BET 2015.
YES.. Jina jingine sio kwenye muziki tena, ni Supermodel wa kwetu kwenye Fashion duniani, Millen Magesse ambaye ameteuliwa kwenye kipengele kipya cha BET ambacho ni BET Global Good Award.
Millen ni nominee pekeyake kwenye Category hiyo.. kwa maana nyingine Tujiandae kumshuhudia akipokea Tuzo hiyo June 28 2015 Los Angeles Marekani.
Tuzo hiyo ni ya heshima kwa Millen kutokana na mchango wake na kujitolea kwenye Jamii.