Burundi kwa sasa iko kwenye vichwa cingi vya habari kutokana na hali ya machafuko ambayo ilijitokeza baada ya Rais Pierre Nkurunziza atangaze uamuzi wa kuwania Urais kwa awamu ya tatu mfululizo.
Jaribio la kutaka kumpindua madarakani wakati akiwa Tanzania kwenye mkutano wa usuluhishi pamoja na Marais wengine wanaounga Jumuiya ya Afrika Mashariki halikufanikiwa na sasa uamuzi uliofikiwa ni kuahirishwa kwa uchaguzi wa Wabunge.
Kingine kilichonifikia leo ni kwamba pamoja na machafuko yanayoendelea nchini humo Rais huyo kaonekana yuko zake uwanjani na wenzake akicheza mpira.