Habari zinasema kwamba Marekani kuna Majimbo kama Alaska, Colorado, Nevada na New York wao wamehalalisha matumizi ya Bangi na mtu anaruhusiwa kuwa nayo kwa kiasi kidogo tu.. Gavana wa Jimbo la Delaware Marekani, Jack Allan Markell kaingia kwenye Headlines leo baada ya kusaini Sheria inayoruhusu matumizi ya bangi.
Kwenye Sheria hiyo mtu wangu huruhusiwi tu kuvuta sehemu ya watu wengi, na kama ukikamatwa umekiuka kanuni hiyo fine yake imepunguzwa pia kutoka Dola 1,150 mpaka Dola 100 tu !!
Jumla ya Majimbo ambayo wamehalalisha kabisa matumizi ya Bangi ndani ya Marekani yako kama 23 hivi mpaka sasa.
March 18 2015 hapahapa nilikusogezea stori kuhusu Jimbo la Colorado ambao walifanikiwa kukusanya kodi ambayo ni Dola Mil. 15 (zaidi ya Bil. 27 Tshs) kutokana na mauzo ya bangi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Toa maoni yako hapa chini kuhusu habari hii