Entertainment

Barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Onyesho la ufunguzi kabla ya fainali kati ya Barcelona na Juventus kuanza
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Alvaro Morata akishangilia baada ya kusawazisha goli la kwanza
Hatahivyo Alvaro Morata alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messi.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.
Suarez akifunga goli la pili
Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu.
                           Furaha ya ushindi: Fc Barcelona baada ya kukabidhiwa taji la ubingwa wa Ulaya




About qwerty

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Top