Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, klabu ya Chelsea, inatarajia kutumia uwanja wa Wembley kwa muda ili kupisha marekebisho ya uwanja wao wa Stamford Bridge.
Chelsea itapewa uwanja wa Wembley kama itakidhi vigezo vilivyotolewa na uongozi husika wa uwanja huo ikiwemo kuhakikisha mashabiki watakaoingia uwanjani hawapungui elfu 50. Mchakato wa marekebisho ya Stamford Bridge yalianza mwaka mmoja uliopita chini ya mmiliki wa klabu hiyo Roman Ibramovich, lengo kuu likiwa ni kuongeza viti ili kuruhusu mashabiki wengi kuingia na kuongeza mapato tofauti na ilivyo sasa ukiwa unaingiza mashabiki elfu 41 tu.