Licha ya kutupwa nje ya michuano ya Copa America na timu ya Paraguay, wachezaji wa kikosi cha Brazil walipokelewa kwa shangwe na mashaiki wa nchi hiyo waliojitokeza kwa wingi uwanja wa ndege kuwalaki wachezaji wao waliokuwa wanarudi kutoka nchini Chilile ambako walitupwa nje ya mashindano hayo kwachangamoto ya mikwaju ya penati na timu ya Paraguay.
Tofauti na ilivyokuwa inanatarajiwa na watu wengi, baada ya kutupwa nje kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwenye bara la Amerika ya Kusini, lakini bado mashabiki walijitokeza kwa wingi kuwapokea wachezaji wao na kupiga nao picha ‘selfies’ mara baada ya kutua kwenye ardhi ya kwao.
Robinho, David Luiz, Willian na Dunga wote kwa pamoja ‘wali-post’ kwenye account zao za mitandao ya kijamii picha mbalimbali walizopiga wakiwa na mashabiki mara baada ya kutua jijini Sao Paulo, Brazil.
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com