Arsenal wamemsainisha mkataba golikipa Petr Cech kutoka Chelsea, Cech mwenye miaka 33 ametua Emirates Stadium kwa mkataba wa muda mrefu (undisclosed) baada ya kudumu Chelsea kwa muda wa miaka 11.
Baada ya kumwaga wino kujiunga na Arsenal, Cech ameandika barua ya kuwaaga mashabiki wa Chelsea kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichokuwa anaitumikia klabu hiyo.
Hii hapa ni barua yake….
Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea sikumoja nitakuja kusema kwaheri kwenye klabu ya Chelsea. Klabu ambayo ilikuwa moyoni kila sekunde tangu nilipojiunga nayo Julai 2004, timu ambayo nifikiri siku moja ningetukika glovu na viatu vyangu na kumaliza safari yangu ya soka nikiitumikia. Lakini mara zote maisha hayako kama unavyofikiria.
Tangu 2004 imekuwa ni safari ya aina yake yenye mafanikio kuliko changamoto, tumeweza kushinda kila aina ya taji lililopo kenye ligi ya England hali kadhalika yale ya Ulaya na lile kubwa kuliko la vilabu bingwa barani Ulaya. Nikitazama nyuma kwenye mafanikio pamoja na msimu wa 2010, nyuma zaidi kwenye mataji ya 2005 na 2006, ushindi wa vikombe viwili cha EPL na FA najivunia sana hilo. Pamoja kama timu tuliandika historia.
Majira ya kiangazi ya msimu uliopita, mambo yalibadilika na nikaelewa sikuwa tena chaguo la kwanza kwenye nafasi ya golikipa lakini nikahisi haikuwa muda muafaka wa mimi kuondoka. Wakati ligi inaendelea ilidhihirika wazi kwamba, hali yangu haingeweza kubadilika na hapo ndipo ninaamini kwa kiwango changu sio mtu wa kuendelea kukaa benchi. Nikafanya maamuzi ya kuondoka kwenda sehemu nyingine kutafuta changamoto mpya.
Kukosa nafasi ya kucheza kulinipa nafasi ya kutuliza akili yangu na kulinifanya nitambue ni kwa kiasi gani nilikuwa nikifurahia kucheza soka kwa kiwango cha juu, kwasababu nafasi hiyo niliikumbuka mno kila mechi ambayo sikupangwa. Nimejitoa kwenye mhezo wa soka na nina njaa ya mafanikiokama ilivyokua tangu mwanzo na ninapenda changamoto zinazoletwa na wachezaji wengine wenye viwango vya hali ya juu ninaokutana nao kwenye Premier League ligi bora na yennye ushindani wa hali ya juu duniani.
Ndio maana niliongea na Bwana Abramovich kuhusu mimi kuendelea kubakia kwenye ligi hii na ninapenda kumshuku toka kwenye uvungu wa moyo wangu kwa ushirikiano alionipa juu ya jambo hili. Inamaana sana kwangu kwasababu bila yeye klabu ya Chelsea isingefika ilipo sasa. Anastahili pongezi nyingi kwa kile alichoifanyia klabu na sisi sote kwa ujumla.
Ninamshukuru kila mmoja anayehusika na klabu ya Chelsea kwa ushirikiano wake, wachezaji, uongozi, benchi zima la ufundi na makocha wote ambao nilifanyanao kazi kwa miaka yote. Bila wao isingewezekana kwetu sote kufikia mafanikio hayo.
Lakini shukrani za dhati ziwaendee mashabiki wote wa Chelsea. Nilifanya kilakitu kwa ajili yenu na ninyi mlirudisha upendo wenu kwangu. Sitosahau kitu hicho kamwe. Kita kaa ndani yangu milele. Tutakutana tena lakini kwa wakati huu nitasimama kwenye goli lingiine. Ninahakika mtaikumbuka historia na kuelewa ni muda sasa wa mimi kuanza maisha mapya.
Ninamtakia kilalakheri kila mmoja kwenye klabu ya Chelsea na nawatakia kilalakheri kwenye msimu mpya ujao na baadae. Asanteni sana kwa miaka 11 ya miujiza.
Petr Cech.
Source: shaffihdauda.com
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com