China iliwahi kupitisha sheria ya kusitisha uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya shule na hospitali lakini haikuweza kutekelezeka kwa mara ya kwanza.
Ingawa kuna baadhi ya nchi kama Jamaica ambapo uvutaji sigara ama bangi si kitu cha ajabu lakini kwa upande wa China sasa kitendo hicho kimeonekana ni kosa kubwa na Serikali imeanza mikakati ya kuhakikisha inatokomeza uvutaji sigara.
Nchi hiyo imerudi kwenye headlines tena na safari hii Serikali imeweka wazi mikakati yake hiyo ya kuzuia uvutaji wa sigara kuanza leo katika maeneo ya wazi hasa ya mji mkuu wa nchini hiyo Beijing na kinyume na hapo kuna faini ambazo zitatolewa kwa wanaokaidi agizo hilo.
Mwonekano wa moja ya packet za sigara zinayouzwa China
Ripoti ya Wizara ya afya imesema nchi hiyo ina wavutaji wa sigara zaidi ya milioni 300,
Sheria hiyo imesema watakaoukiuka makubaliano hayo watatozwa faini ya fedha ya China yuan 32.25 ambayo ni sawa na dola 1.60 huku watakaorudia kosa hilo kwa zaidi ya mara tatu watatozwa faini ya dola 1600 pamoja na kuwekwa kwenye website ya Serikali.
Pia Serikali imetoa onyo kwa wauzaji wa sigara kuhakikisha wanauza kuanzia mita 100 kutoka katika ameneo ya wazi na karibu na shule ama hospitali ili kukwepa faini hizo