Hii haiwezi kuhitimisha tetesi za David De Gea kujiunga na Real Madrid majira haya ya kiangazi, lakini inatia moyo kwa kiasi kikubwa hususani kwa mashabiki wa Manchester United.
Leo Gazeti la Marca (tazama picha chini) limekuja na stori kwenye ukurasa wake wa Mbele ikiwa na picha ya David De Gea na Bosi wa Manchester United, Lois van Gaal yenye kichwa cha habari “Siempre Negativo” – “Always Negative”.
De Gea amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Man United na kwa miezi mingi amekuwa akihusishwa kutua Real Madrid.
Marca wameripoti kwamba Louis van Gaal anajitahidi kadri awezavyo kuzuia mpango wa Real Madrid kumsajili golikipa huyo namba moja Old Trafford.
Gazeti hilo linasema kwamba kutokana na ugumu uliopo , Real Madrid wameshaanza kuangalia mpango wa pili ambao ni kumsajili kipa wa Leverkusen, Bernd Leno ili kurithi mikoba ya Casillas.
Marca mara zote wamekuwa kama wasemaji wa Real Madrid, lakini sasa inashangaza kwa taarifa hiyo hasi waliyochapisha kuhusu miamba ya Bernabeu, tena ukurasa wa mbele.
Habari hizi ni nzuri kwa mashabiki wa Manchester United
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com