Zilianza tetesi za hapa na pale lakini hakukua na neno lolote linalomhusisha Zlatan moja kwa moja lakini hivi sasa mambo yamekua tofauti kidogo.
Baada ya kushinda Quadruple na PSG, Zlatan anatafuta nafasi nyingine na kushinda Champions League kwenye misimu inayokuja. Kuhusu Super Swedish striker imeripotiwa kwamba hivi sasa yupo wazi kurudi AC Milan, ila ameacha tu nafasi kwa AC Milan kuishawishi PSG kuumuza kwao.
Kutokana na AC Milan kuwa na muwekezaji mpya kutoka Thailand kuna uwezekano mkubwa kwa AC Milan kuweza kumnunua Zlatan na kurudisha majeshi kwenye kikosi chao.
AC Milan wana mipango mikubwa kwa ajili ya msimu ujao ili waweze kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani na nje ya Italy