Entertainment


Manchester United wameshinda vita ya kumsajili nyota wa Monaco, Radamel Falcao.
Falcao ameanguka wino leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili kwa Ligi Kuu ya Uingereza kukipiga na Mashetani wekundu kwa mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo.
Mshambuliaji huyo nyota ataigarimu Man U kitita cha paundi milioni 12 sawa na fedha za madafu za bongo Bilioni 32.5.
Falcao atashuka katika dimba la Old Trafford kuungana na nyota wengine waliojiunga na klabu hiyo Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo wakiwa chini ya meneja wao Louis van Gaal.


Falcao  mwenye asili ya Colombia mwenye umri wa miaka 28 huenda akaibuka na kitita cha shilingi Milioni 543 kwa wiki. 

Mchezaji huyo alikuwa akiwaniwa pia na timu za Manchester City na Arsenal. Man U ilikuwa ikimuwania mshambuliaji huyo kuziba pengo la majeruhi Robin van Persie ambapo pia kuwasajiliwa kwa Falcoa kumewauza wachezaji Danny Welbeck huku Javier Hernandez akienda Real Madrid.

Baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili Falcao atarudi kujiunga na kikosi chake cha timu ya taifa ambacho kinajiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Brazili utakao pigwa Ijamaa hii




About qwerty

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Top