MSHAMBULIAJI Javier Hernandez ametambulishwa rasmi jijini Madrid na kupewa Jersey No. 14 ambayo ni namba aliyovaa alipokua manchester United. Pia Real Madrid wana mtazamo wa kumnunua kabisa mchezaji huyu kutoka Manchester United kwani kwa sasa yuko Real Madrid kwa mkopo.
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni 1.5.
Chicharito alipokua kwenye vipimo vya afya
Javier 'Chicharito' Hernandez akitia sign mkataba jijini Madrid