Dirisha
la usajili barani ulaya limefungwa usiku wa jana – Shinji Kagawa ni
mmoja wa wachezaji waliofanya uhamisho katika dirisha hili la usajili.
Kiungo wa Japan, aliuzwa kutoka Manchester United kwenda Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £6.3million.
Fedha hizo
walizolipa Dortmund zinaweza kuwa zimerudi ndani ya siku kadhaa baada ya
ripoti ya gazeti la BILD kusema kwamba mauzo ya jezi namba 7
atakayoivaa Kagawa akiwa Dortmund yamekuwa ya kasi mno.
Ripoti zinasema
jezi ya Shinji Kagawa iliuzwa mpaka kufikia idadi ya jezi 5,000 katika
kipindi cha masaa kadhaa tangu alipotangazwa rasmi kurudi kwenye klabu
yake hiyo aliyohama na kwenda United mnamo mwaka 2010.