Wiki mbili baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Uingereza, dirisha la usajili barani ulaya limeanza kushika hatamu.
Klabu ya Liverpool leo hii imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo James Milner kutoka Manchester City.
Milner mwenye umri miaka 29, alipiga chini nafasi ya kuendelea kubaki Etihad Stadium ili awese kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya Brendan Rogers msimu ujao.
Milner amemaliza mkataba wake na City, na atajiunga rasmi na Liverpool tarehe 1 mwezi ujao.
Mchezaji huyo alijunga na City akitokea Aston Villa miaka minne iliyopita na amefanikiwa kutwaa makombe mawili ya Ligi kuu ya Uingereza pamoja na FA Cup.
Toa maoni yako hapa chini kuhusiana na habari hii.
Toa maoni yako hapa chini kuhusiana na habari hii.