Kwenye headlines toka Dodoma labda hii ilikupita, Wabunge wamesikika mara nyingi wakilalamika kwamba Serikali itafanya maisha yawe magumu baada ya kutangazwa kwamba bei ya mafuta itabidi ipande ili kuchangia miradi ya usambazaji wa umeme TZ.
Africanjam, We provide news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Breaking news. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com
“Uchumi wako utategemea mchango wako unaoutoa katika Taifa hili… Tukiona wafadhili wanatusaidia ni kwa sababu wanachukua Kodi ya mwananchi wa kule wanakuja kutusaidia. Kama tuna uchungu wa nchi hii ni lazima mwananchi achangie shilingi mia moja yake ili tumpelekee umeme kule aliko“>>> Saada Mkuya.
“Hatuwezi kupitisha bakuli kwa wafadhili tukaomba fedha ili tupeleke umeme vijijini.. Kama tunataka maendeleo ya kiuchumi ya Mwananchi hii tozo tumeipendekeza tunaomba Wabunge mtusapoti kwenye hili“
“Ni lazima mwananchi achangie maendeleo ya nchi yake.. Tunaomba shilingi mia kwa kila ya mafuta ya taa, petroli na diesel kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini… Hesabu zetu zimeonesha katika tozo hii tutapata shilingi Bilioni 276.. Tukitegemea fedha za wafadhili katika kutekeleza miradi ya maji inawezekana tusifike tunakotaka kufika”>>> Saada Mkuya.