Klabu ya Liverpool imetangaza kufikia makubaliano na klabu ya Burnley juu ya usajili wa mshambuliaji wa England, Danny Ings.
Kikosi cha Liverpool
msimu uliopita kimejikuta kikishindwa kufikia malengo yake baada ya
kumaliza nje ya nafasi za kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa imekuwa
ikihaha kuhakikisha inasajili wachezaji ambao wanaweza kuendana na
malengo na ukubwa wa klabu hiyo, japo mchezaji Danny Ings amekuwa kwenye orodha ya kocha Brendan Rogers kwa muda mrefu.
Danny Ings amefunga mabao 11 kwenye msimu uliopita wa EPL.
Kinyume na hali ilivyokuwa kwa klabu yake ya Burnley ambayo imeshuka daraja Danny Ings
alikuwa na msimu mzuri kwake binafsi akiwa ametokea kuwa moja kati ya
washambuliaji tishio kwenye ligi kuu ya England baada ya kufunga mabao
11.
Ings pia alikuwa anatafutwa na klabu kadhaa ndani ya England na Ulaya ambapo kwa nyakati tofauti Manchester United na Real Sociedad ya Hispania zimekuwa zikihaha kusaka saini yake.
Ujio wa Ings huenda ukawa unamaanisha mwisho wa washambuliaji Mario Balotelli na Rickie Lambert ambao walishindwa kuonyesha ubora baada ya kusajiliwa msimu uliopita.