Timu ya Taifa ya Argentina imetinga kwa kishindo hatua ya fainali ya Copa America baada ya kuitandika Paraguay kipigo cha mbwa mwizi cha magoi 6-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Marcos Rojo (15), Javier Pastore (27), Angel Di Maria (47, 53), Sergio Aguero (80) na Gonzalo Higuain (83), huku goli la kufutia machozi kwa Paraguay likifungwa na Lucas Barrios (43).
Kama kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anataka kupata kiwango cha Di Maria, labda amsajili Lionel Messi na kama anashindwa kufanya hivyo, basi amnase Javier Pastore.

Hawa watu walimfanya Di Maria apige soka la kiwango cha juu kutokana na pasi maridhawa walizokuwa wanammegea.
Messi alionesha kiwango kizuri na kujaribu kufunga mara kadhaa, lakini bahati haikuwa upande wake.
Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.
Follow us on Twitter @african_jam
Like our Facebook page Africanjam.com