Entertainment


Radamel Falcao amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Chelsea na ataungana na timu yake mpya kwenye ziara ya kujiandaa na msimu ujao (pre-season) huko bara la America ya Kaskazini hii ni kwa muji wa ripoti.
Mjomba pamoja na baba yake Falcao wamethibitisha kwamba, mkataba umeshasainiwa kati ya mshambuliaji huyo na klabu ya Chelsea.

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, Chelsea wamekubaliana na Monaco kumsajili Falcao kwa mkopo wa mwaka mmoja lakini mkataba huo unakipengele cha kumsajili moja kwa moja msimu ujao.
Chelsea bado hawajatangaza rasmi kumsajili Falcao lakini walikuwa na mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendez kwa takribani wiki tatu ili kuhakikisha wanamsajili Falcao licha ya kwamba mshahara wake unagharimu kiasi cha pauni 265,000 kwa wiki.
The Guardian limeripoti kuwa, mabingwa hao wa ligi ya England wakotayari kumlipa Falcao kitita cha pauni 180,000 kwa wiki na pauni milioni 4 kama ada ya uhamisho.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema atamsaidia Falcao kurudia makali yake ya zamani baada ya kuwa na msimu mbovu alipokuwa Manchester United kufuatia jeraha la goti la mudamrefu.



Africanjam is website that came into service December 2013(with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports, Entertainment as well as Technology tips and some Amazing Facts. We also provide Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.


Follow us on Twitter @african_jam 
Like our Facebook page Africanjam.com




About qwerty

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Top