Entertainment

Rais  John Pombe Magufuli leo  Januari 7, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika mkutano huo Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
1
Rais Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa Ikulu
Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.
5
Naye Jaji Warioba amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.
“Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo” Jaji Warioba.
Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu
4
Source: www.millardayo.com

Africanjam is website that was launched  in December 2013 (with another domain) and on April 2014 the new domain Africanjam(dot)com came into use. It was found by John Kapela who is currently in Dar es Salaam Tanzania. This site provides news from Africa and all over the world in Politics, Sports and Entertainment. We also provide Technology tips, some Amazing Facts as well as Football updates from all over the world. Visit this site everyday for being in touch with everything happening in Africa and the whole world.

Follow us on Twitter @african_jam 

Like our Facebook page Africanjam.com




About qwerty

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Top